vendredi 7 juin 2013

Miss World 2013: Hakutakuwa na vazi la bikini katika shindano la kumsaka mrembo wa dunia mwaka huu!

Shindano la kumtafuta mrembo wa dunia kwa mwaka huu 2013 linategemewa kufanyika huko
Indonesia, lakini utofauti utakaokuwepo ni kwamba washiriki hawatavaa vazi la bikini kama
ilivyozoeleka katika mashindano yaliyopita.

Kwa mujibu wa mtandao wa aceshowbiz waandaaji wa shindano hilo la mrembo wa dunia 2013
wametoa taarifa ya uamuzi huo Jumanne wiki hii (June 5) ikiwa ni hatua ya kuepukana na
kutofautiana na vikundi vya kiislam vya Indonesia ambayo aslilimia 90 ya wananchi wake ni
waislam.
Msemaji wa RCTI waandaaji rasmi wa Miss World 2013 nchini Indonesia, Adjie S. Soeratmadjie
alisema
“Kutakuwa hakuna bikini katika shindano la miss world mwaka huu ili kuheshimu mila zetu za jadi
na maadili, Hili ni suala nyeti hapa Indonesia.. Tumejadiliana tangu mwaka jana na wamekubali.”
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika mwezi september mwaka huu (2013).

0 commentaires:

Maoni yako yanaweza tusaidia tunakuskia!