DIAMOND PLATNUM FREE PERSON FROM UMASIKINI
SIRI imefichukua kuwa madai kwamba
‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’
ni memba wa jamii ya siri inayodaiwa kumwabudu shetani, Freemason
a.k.a Wajenzi Huru zilianza kitambo lakini sasa zimeshika kasi baada
ya kunaswa kwa picha inayomuonesha akisalimiana na mtasha kwa ishara
ya Kifreemason, Ijumaa Wikienda linaibumburua. Kwa mujibu picha hiyo,
tukio hilo lilijiri nchini Uingereza, mwaka jana, Diamond alipokwenda
huko kwa ajili ya shoo. MAVAZI Ilidaiwa pia kuwa mavazi ya Diamond
(meusi)
yalishabihiana sawia na yale ya mtasha huyo yanayoelezwa kuwa
sehemu ya mavazi ya jamii ya Freemason. ISHARA Kingine kilichoibua
maswali ni ishara ya salamu ya wawili hao ambayo ilitengeneza nembo
ya Freemason ya ‘V’ au bikari kwa namna walivyogusana kwa vidole.
Kwa mujibu wa wadau walioiona picha hiyo iliyonaswa kwenye mtandao wa
Twitter, Diamond amekuwa na ishara nyingine nyingi za aina hiyo hivyo
kuzidi kuzua utata kama ni memba wa jamii hiyo. “Lakini inawezekana
kwa sababu nasikia ukishajiunga unapata mafanikio ya ghafla. ‘So’
kuhusu hili, sina upande wa kusimamia,” ilisomeka sehemu ya maoni
kwenye mtandao huo baada ya kuibuka mjadala mzito juu ya ishu hiyo
inayozidi kushika kasi mithili ya moto wa kifuu. “Tungeshukuru kama
Diamond mwenyewe angejitokeza aseme ukweli kwani akinyamaza anazidi
kutuweka njia panda,” ilisomeka sehemu nyingine ya maoni hayo huku
ikiungwa mkono na wengi. UNATAKA KUMSIKIA DIAMOND? SOMA HAPA Ili
kumaliza utata wa je, Diamond ni Freemason au la,mzee wa chimbo
lilibeba jukumu la kumtafuta ili aanike ukweli wake ambapo alikuwa na
haya ya kusema: “Unajua mwanzoni nilikuwa sikumbuki ni lini na wapi
nilipiga picha ya dizaini hiyo. ‘Anyway’, isiwe kesi, nakumbuka
ilikuwa Uingereza kipindi kile nilikuwa na shoo nchini humo.
“Nakumbuka walinifuata watasha wengi tofauti lakini huyo mmoja
alining’ang’ania sana nipige naye picha. “Kwa kweli
alinilazimisha sana kwa sababu mwanzo nilikataa lakini baadaye
nikaona isiwe ishu nikampa ushirikiano alioutaka. “Mimi sikuona
matatizo alivyotaka tusalimiane kwa kugusisha vidole kwa sababu
nilikuwa sijui chochote kuhusu Freemason. Nimeijua baada ya mambo
haya kuyasikia kwa sana hivi karibuni. “Kwa hiyo inawezekana siku
hiyo waliniunganisha bila mimi kujua (kicheko).” SASA UKWELI NI
UPI? Mara kadhaa Diamond amekuwa akihusishwa na Freemason kutokana na
mafanikio ya ghafla aliyoyapata na mvuto alionao kwa mashabiki wake
ndani na nje ya Bongo.mzee lilipotaka kupata ukweli kutoka kwake,
Diamond alifunguka: “Si kweli bwana, mimi nazisikia tu hizi habari
kama wengine. Nasikia tu ipo hapa Bongo na kiongozi wake ni Sir Andy
Chande, zaidi ya hapo sijui chochote. “Mimi ni mtu wa swala tano na
mafanikio yangu naamini Mungu ndiyo kila kitu.” KUNA MSANII
MWINGINE Mbali na mwigizaji Jacqueline Wolper na marehemu Steven
Charles Kanumba ‘The Great’ ambao wamekuwa wakitajwatajwa na
mambo ya Ufreemason,
0 commentaires:
Maoni yako yanaweza tusaidia tunakuskia!