MWANA FA AVUNA MILIONI 18 NDANI YA MIEZI MITATU KWENYE RINGBACK TONE
Kwa mujibu wa Mwana FA
mwenyewe ambaye leo ameachia wimbo wake mpya, Kama Zamani, hivi
karibuni alipokea malipo ya miezi mitatu kutoka kampuni moja ya kuuza
miito ya simu aka RBT yanayofikia shilingi za kitanzania milioni 18.
Akiongea leo kwenye
kipindi cha XXL cha Clouds FM, FA aliyekuwa wa tatu kati ya wasanii
waliopata fedha nyingi zaidi kwenye malipo hayo chini ya Rose Mhando
na Diamond, amesema ameamua kuweka wazi hilo ili watu waondoe imani
kuwa muziki wa hip hop hauuzi.
Tarehe 31 mwezi huu, Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma atakuwa na show yake aliyoipa jina, The Finest.
Tarehe 31 mwezi huu, Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma atakuwa na show yake aliyoipa jina, The Finest.
Editing by NadavCom Vision
0 commentaires:
Maoni yako yanaweza tusaidia tunakuskia!